LifeStyle

Videon Vixen wa Vaileti ya Matonya Aomba Msaada wa Kujinasua Umaskini

Videon Vixen wa Vaileti ya Matonya Aomba Msaada wa Kujinasua Umaskini

Mwanadada aliyewahi kuwa video vixen kwenye wimbo wa Matonya wa Vaileti amefunguka kuhusu changamoto zinazomkabili baada ya kujitokeza wazi na kuomba msaada wa kujinasua kutoka kwenye lindi la umaskini.

Akizungumza kwenye mahojiano hivi karibuni, ameeleza kuwa ushawishi wa marafiki na makundi mabaya ulimpelekea kupoteza mwelekeo wa maisha na kujikuta akipambana na hali ngumu kiuchumi kutokana na uraibu wa dawa za kulevya.

Mrembo huyo ambaye kwa sasa ni mama ya watoto wawili, amesema sasa yuko tayari kubadilika na kuanza upya, huku akiwatahadharisha vijana kuhusu kuchagua marafiki sahihi.

Aidha, ameomba mashabiki wa msanii Matonya na Watanzania kwa ujumla msaada wa kifedha ili aweze kusimama tena na kuachana na uraibu wa pombe ambao umekuwa kikwazo kikubwa kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *