Msanii wa Arbantone VJ Patello amedai kuwa hahitaji muziki ili kuishi au kufanikisha maisha yake.
Akizungumza kwenye mahojiano yake hivi karibuni, msanii huyo ameweka bayana kuwa muziki si msingi wa maisha yake, akisema kuwa anaweza kuishi na kufanikiwa hata bila kuendelea na muziki.
Patelo, amewataka watu wanaofuatilia kukoma na kuendelea na shughuli zao bila kujihusisha na maisha yake binafsi. Ameeleza kuwa kile anachokifanya kwa sasa hakimhusu mtu yeyote na hakihitaji maoni ya watu.
Kauli yake imekuja mara baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuachia wimbo wowote katika siku za hivi karibuni.