Gossip

Bahati na Diana B Wazima Tetesi za Kuachana kwa Kuonekana Pamoja Kwenye Klabu

Bahati na Diana B Wazima Tetesi za Kuachana kwa Kuonekana Pamoja Kwenye Klabu

Mwanamuziki kutoka Kenya, Bahati na mke wake Diana Marua, wameonekana wakifurahia burudani pamoja siku chache tu baada ya kuzuka kwa tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao, jambo lililozua gumzo kubwa mitandaoni.

Kupitia video inayosambaa mtandaoni, wawili hao wameonekana wakiwa kwenye moja night club katika hali ya furaha, wakicheka na kusherehekea pamoja, hali iliyozima uvumi uliokuwa umeenea kuwa ndoa yao inasuasua.

Uvumi wa kuvunjika kwa ndoa ulianza baada ya mashabiki kugundua kuwa Bahati na Diana walikuwa wameachana kufuatana (unfollow) kwenye akaunti zao za Instagram, hatua iliyotafsiriwa na wengi kama ishara ya mgogoro katika ndoa yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *