WhatsApp imeanza kujaribu mpango mpya wa subscription ya kulipia, hatua inayolenga kuwapa watumiaji uwezo wa kupata huduma na vipengele vya ziada tofauti na vilivyopo kwa sasa.
Kupitia mpango huu, watumiaji watakaolipia wataweza kufurahia baadhi ya features maalum zikiwemo stickers za premium, themes za kipekee, uwezo wa ku-pin chat zaidi ya tatu, ringtone maalum kwa chats, pamoja na icon mpya za WhatsApp na badge kwenye profile zao. Aidha, mpango huu utawezesha watumiaji kuepuka matangazo kwenye sehemu ya Status.
Kwa sasa, mabadiliko haya yako katika hatua za mwanzo za majaribio na yanapatikana kwa idadi ndogo ya akaunti ambazo zipo kwenye waitlist. WhatsApp bado inaendelea ku-test concept na features husika, na bei ya subscription bado haijatangazwa rasmi.
Inatarajiwa kuwa katika miezi ijayo, WhatsApp itaanza kutekeleza mabadiliko haya rasmi kwa watumiaji wengi zaidi endapo majaribio yataonyesha mafanikio. Hatua hii inaashiria mabadiliko makubwa katika mkakati wa WhatsApp, huku ikilenga kuongeza vyanzo vya mapato bila kuathiri matumizi ya msingi ya huduma kwa watumiaji wa kawaida.