Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Zuchu, ameshindwa kuficha mapenzi yake kwa msanii nyota Diamond Platnumz kupitia ujumbe wa mahaba aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram wakati wa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Diamond.
Katika ujumbe wake, Zuchu amemtakia Diamond kheri ya siku ya kuzaliwa huku akimpa heshima kama msanii, kiongozi na mpenzi. Ameweka wazi hisia zake akimtaja Diamond kwa majina ya mahaba ikiwemo Shmugum wangu, Kiboko yangu, Boss wangu, Hero wangu, Mentor wangu, Msimamizi wangu, Danga langu, Last Say wangu, Muchuchu wangu, Boyfriend na Mume wangu.
Zuchu pia ameeleza kuwa ataendelea kusimama naye kwa hali na mali, akimtaka ajiandae kisaikolojia kwa changamoto na mapenzi yao ya milele. Aidha, amemtakia maisha marefu yenye furaha huku akimtaja kama msanii bora zaidi wa kizazi chake (GOAT)
Kupitia utani wa kimahaba, Zuchu amemkumbusha Diamond kuwa zawadi aliyo nayo kubwa zaidi ni yeye mwenyewe, na hivyo hana haja ya zawadi nyingine zaidi ya kumrudishia zile alizowahi kuchukua.