Msanii nyota wa muziki kutoka Kenya, Willy Paul, ameweka rekodi mpya kwenye jukwaa la muziki la Boomplay baada ya kutajwa kuwa msanii wa kiume anayesikilizwa zaidi kwenye mtandao huo.
Willy Paul amefikisha jumla ya wasikilizaji milioni 107 huku wimbo wake “Keki” aliomshirikisha Bahati ukitajwa kuwa wimbo uliosikilizwa zaidi mwaka 2025.
Kupitia mitandao ya kijamii, msanii huyo amewashukuru mashabiki wake akisema wameendelea kumuunga mkono kwa dhati, jambo lililomfikisha kileleni katika safari yake ya muziki.
Rekodi hii mpya inaongeza orodha ya mafanikio ya Willy Paul na inaonyesha wazi kuwa bado ni mmoja wa wasanii wenye nguvu kubwa katika soko la muziki wa kidijitali nchini Kenya na kanda ya Afrika Mashariki.