Mwimbaji kutoka Ghana, Fantana, amemwonya staa wa muziki wa Tanzania, Diamond Platnumz, baada ya kudaiwa kulitaja jina lake wakati wa tamasha lake la hivi karibuni jijini Lagos, Nigeria.
Kupitia Instagram Story, Fantana amehoji sababu ya Diamond kuendelea kulitaja jina lake hadharani ilhali anadaiwa kuwa na furaha katika ndoa yake. Amesema hatua hiyo si ya lazima na inaonyesha kukosa heshima, hasa ikizingatiwa kuwa tamasha hilo lilihudhuriwa na mashabiki wengi.
Fantana amemtaka Diamond aache kabisa kulitaja jina lake na kuliacha lipumzike, akisisitiza kuwa hataki kuhusishwa naye kwa namna yoyote hadharani.
Kauli hiyo imeibua mjadala mitandaoni, huku mashabiki wakitofautiana iwapo maneno ya Diamond yalikuwa mzaha wa jukwaani au jaribio la makusudi la kutafuta kiki.