Gossip

Akothee Amjibu Shabiki Aliyedai Alimpotezea Nelly Oaks Muda

Akothee Amjibu Shabiki Aliyedai Alimpotezea Nelly Oaks Muda

Mwanamuziki na mfanyabiashara Akothee amemjibu kwa hasira shabiki aliyetoa maoni mtandaoni akidai kuwa alimharibia aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Nelly Oaks, muda wa ujana wake na kumtaka atafute mke ili asalie watoto kabla hajachelewa.

Shabiki huyo alidai kuwa Nelly Oaks anapaswa kuendelea na maisha yake na kujenga familia mapema, akihusisha uhusiano wake wa zamani na Akothee kama sababu ya kupoteza muda.

Akothee hakuvumilia kauli hiyo na aliibuka kumkemea shabiki huyo kwa kumhusisha Nelly katika mjadala huo. Amehoji kwa nini jina la Nelly linavutwa katika mazungumzo hayo na kusisitiza kuwa ana heshima kubwa kwake.

Aidha, ameeleza kuwa si sahihi kwa watu wa nje kudhani wanajua mipango au maamuzi ya maisha ya Nelly Oaks, akiuliza ni nani aliyesema hana au hatakuwa na mke na watoto..

Akothee na Nelly Oaks waliwahi kuwa katika uhusiano uliovuta hisia za wengi kabla ya kutengana, lakini wameonekana kudumisha heshima ya pande zote hata baada ya kuachana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *