LifeStyle

Nadia Mukami awajibu wakosoaji wa mwonekano wake baada ya kujifungua

Nadia Mukami awajibu wakosoaji wa mwonekano wake baada ya kujifungua

Msanii wa muziki Nadia Mukami amewajibu wakosoaji waliotoa maoni kuhusu mwonekano wake, wakidai amenenepa kupita kiasi baada ya kujifungua mtoto wake wa pili.

Kupitia kurasa zake za kijamii, Nadia ameweka wazi kuwa mashabiki wanapaswa kuuzoea mwonekano wake wa sasa hadi mtoto wake atakapofikisha mwaka mmoja.

Msanii huyo wa watoto wawili, amesema kuwa yuko sawa na mwili wake wa sasa na hana presha ya kubadilika kwa ajili ya kuridhisha maoni ya watu mtandaoni.

Kauli ya Nadia imekuja mara baada ya picha na video za shoo yake ya Nyali kusambaa mtandaoni, hatua ambayo ilipelekea baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kumshauri apunguze uzito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *