Entertainment

Akothee Atoa Rate Card Rasmi kwa Matukio na Deals za Kibiashara

Akothee Atoa Rate Card Rasmi kwa Matukio na Deals za Kibiashara

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Akothee, ameachia rasmi rate card yake, ikionyesha gharama za kum-book kwa shughuli mbalimbali za burudani na ushirikiano wa kibiashara.

Kwa mujibu wa taarifa alizochapisha mtandaoni, Akothee anatoza KSh 700,000 kwa kuhudhuria hafla bila kutumbuiza. Hii ni kwa matukio kama mikutano ya kibiashara, sherehe binafsi au hafla za kitaasisi ambapo uwepo wake pekee unahitajika.

Kwa upande wa maonyesho ya moja kwa moja (live performances), bei yake inaanzia KSh 1.2 milioni hadi KSh 1.5 milioni, kutegemeana na aina ya hafla, maandalizi ya jukwaa na mahitaji ya tukio husika.

Aidha, Akothee anatoza KSh 2 milioni kwa ground activations, pamoja na KSh 2 milioni kwa mwezi kwa mikataba ya brand ambassadorship na shughuli za masoko (Marketing).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *