Msanii nyota wa muziki nchini Kenya, Bahati, ametangaza kuwa yeye ndiye msanii mwenye mafanikio makubwa zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Bahati ametoa kauli hiyo alipokuwa akiwatakia mashabiki wake sikukuu njema ya Krismasi, akiwa pamoja na mke wake Diana B na watoto wao, akisema safari yake ya muziki imejaa baraka, mafanikio na ushindi mkubwa unaoonekana wazi kupitia maisha na kazi zake.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya msanii huyo kujizawadia gari la kifahari aina ya Range Rover, kama sehemu ya kusherehekea kutimiza miaka 33 tangu kuzaliwa kwake.
Kupitia mitandao ya kijamii, Bahati alishiriki picha na video za gari hilo, akisema ni zawadi ya kujithamini na kuthamini juhudi zake binafsi.