Tech news

TikTok Yaongeza Sehemu Mpya ya Kutuma Cards Kwenye DM

TikTok Yaongeza Sehemu Mpya ya Kutuma Cards Kwenye DM

Mtandao wa kijamii wa TikTok umeendelea kuja na maboresho mapya kwa watumiaji wake. Safari hii, TikTok imeongeza kipengele kipya kinachowaruhusu watumiaji kutuma Cards kupitia ujumbe binafsi, maarufu kama DM.

Kupitia kipengele hiki kipya, mtumiaji anaweza kutuma card inayofanana na kadi ya kawaida ya kuandikia ujumbe mfupi. Ujumbe huo hujificha ndani ya card, na mpokeaji atalazimika kuifungua kwanza ndipo aweze kusoma ujumbe uliomo.

Ubunifu huu unaifanya mawasiliano yawe ya kuvutia zaidi, kwani badala ya ujumbe wa kawaida, sasa kuna mshangao mdogo kabla ya ujumbe kusomwa.

TikTok imeeleza kuwa lengo la kuongeza kipengele hiki ni kuboresha uzoefu wa mawasiliano ya faragha na kuwapa watumiaji njia mbadala ya kujieleza kwa ubunifu zaidi.

Kwa sasa, kipengele hiki kinaendelea kupatikana kwa watumiaji mbalimbali, huku TikTok ikiendelea kufanya maboresho zaidi ya huduma zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *