Entertainment

Miss P Afunguka Kuhusu Kuacha Muziki

Miss P Afunguka Kuhusu Kuacha Muziki

Aliyekuwa msanii wa lebo ya Saldido International, Miss P, amefunguka kwa hisia kali kuhusu kujiondoa kwake ghafla kwenye tasnia ya muziki.

Kupitia TikTok Live iliyojaa majonzi, msanii huyo ameeleza kuwa umaarufu wa ghafla ulimlemea akiwa bado mdogo sana. Amesema alijikuta katika mazingira magumu ya tasnia ambayo hakuyafahamu vyema kutokana na umri wake mdogo, hali iliyowafanya baadhi ya watu kumtumia vibaya.

Msanii huyo, ameongeza kuwa licha ya kuendelea kutoa kazi chini ya Saldido, mazingira ya kazi yalizidi kuwa sumu na hatimaye kumfanya achoke kabisa.

Miss P alipata umaarufu mkubwa mwaka 2021 baada ya kuachia wimbo wa Liar aliomshirikisha bosi wake Willy Paul. Mafanikio hayo yalimfungulia milango ya kutoa ngoma nyingine zilizopokelewa vyema kama Mashallah, Fall In Love na Popo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *