Tech news

China Yaweka Sheria Kali Dhidi ya Usukani wa Kisasa wa Yoke

China Yaweka Sheria Kali Dhidi ya Usukani wa Kisasa wa Yoke

China imetangaza rasmi mpango wa kupiga marufuku matumizi ya usukani wa aina ya yoke yaani usukani usio na mviringo kamili, ikisema muundo huo unaweza kuongeza hatari ya majeraha kwa dereva wakati wa ajali.

Uamuzi huo umetolewa kupitia rasimu ya viwango vipya vya usalama kutoka Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China, maarufu kama MIIT.

Katika maelezo yake, MIIT imesema usukani wa aina ya yoke unaweza kupunguza uthabiti wa dereva kuushika vizuri wakati wa dharura, na pia kuongeza hatari ya majeraha endapo ajali itatokea.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, kanuni hizo mpya zitaanza kutumika rasmi kuanzia Januari Mosi, mwaka 2027.

Usukani huo ulipata umaarufu mkubwa mwaka 2021 baada ya kampuni ya Marekani ya kutengeneza magari ya umeme, Tesla, kuanza kuutumia kwenye baadhi ya magari yake ya kisasa. Baadaye, kampuni nyingine ikiwemo Lexus pia zilianza kuujaribu katika baadhi ya masoko duniani.

Hatua ya China inatarajiwa kuathiri watengenezaji wa kimataifa wanaouza magari yao katika soko hilo, ambalo ni miongoni mwa masoko makubwa zaidi ya magari duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *