Entertainment

KRG The Don Atawazwa Msanii Bora wa Dancehall Kenya C Awards

KRG The Don Atawazwa Msanii Bora wa Dancehall Kenya C Awards

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Kenya, KRG The Don, ametawazwa rasmi kama Msanii Bora wa Dancehall wa Mwaka katika tuzo za Kenya C Awards.

Kupitia mitandao ya kijamii, msanii huyo ameshukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono na kusema ushindi huo ni uthibitisho wa juhudi, kazi ngumu na kujituma kwake katika kukuza muziki wa dancehall nchini kwao Kenya.

Msanii huyo ambaye watu wamekuwa wakimchukulia poa, amesema kuwa tuzo hiyo ni ya mashabiki wake waliompa sapoti tangu mwanzo wa safari yake ya muziki.

Hafla ya utoaji tuzo za Kenya C Awards huwaleta pamoja wasanii, watayarishaji na wadau mbalimbali wa tasnia ya burudani nchini Kenya kwa lengo la kutambua na kusherehekea vipaji vinavyoibuka na vile vilivyojizolea umaarufu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *