Msanii wa muziki wa Bongo Flava Dudu Baya amekanusha madai yaliyoibuliwa na Mr Nice kwamba aliwahi kupigwa na kikosi cha mizinga hadi kufikia hatua ya kufuliwa nguo.
Akizungumzia sakata hilo, Dudu Baya amesema madai hayo ni ya uongo na hayana ukweli wowote, akisisitiza kuwa hajawahi kupigwa na mtu yeyote. Ameeleza kuwa hata kipindi anamshushia Mr Nice kichapo, mabouncer walikimbia na watu pekee waliomdhibiti ni askari polisi waliofika eneo la tukio.
Kwa mujibu wake, tukio linalozungumziwa Mr. Nice labda ni lile lililotokea alipokwenda kumsaidia Chid Benz baada ya kuvamiwa klabuni. Dudu Baya amedai kuwa katika purukushani hiyo, aliingia klabu hapo kumuokoa Chid Benz kutoka mikononi mwa wahuni bila kupigwa kama inavyodaiwa.
Aidha, amedai kuwa hata Kalapina pamoja na washikaji zake wanashangazwa na madai ya Mr Nice, wakiamini kuwa ni simulizi za kutunga kwa ajili ya kutafuta kiki mtandaoni.