Entertainment

Diamond Atuhumiwa Kuiga Ubunifu wa Alikiba na Mbosso Kwenye Wimbo wake Mpya

Diamond Atuhumiwa Kuiga Ubunifu wa Alikiba na Mbosso Kwenye Wimbo wake Mpya

Staa wa muziki barani Afrika Diamond Platnumz ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya kudaiwa kuiga ubunifu wa baadhi ya mastaa wa Bongofleva na kuutumia kwenye wimbo wake mpya uitwao, Natulizana.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa masuala ya muziki, scene inayomuonesha Diamond akiwa jangwani ndani ya gari la wazi akiwa na mwanamke, inafanana na video ya Ova ya Mbosso kuanzia muonekano wa mandhari, mpangilio wa picha na hali ya kimahaba.

Aidha, mjadala mwingine umeibuka kuhusu upande wa sauti. Baadhi ya wachambuzi wa muziki mtandaoni wanadai kuwa melody ya kiitikio cha Natulizana inafanana na mtiririko wa sauti uliotumika na Alikiba katika wimbo Dah aliomshirikisha Nandy. Wanaodai hivyo wanasema ladha ya kiitikio hicho ina muundo unaokaribiana na ule wa wimbo huo wa awali.

Hata hivyo, wapo wanaotetea kuwa kufanana kwa baadhi ya vipengele si ushahidi wa kuiga, bali ni matokeo ya wasanii kufanya kazi ndani ya mtindo mmoja wa muziki wa Bongo Flava, ambao mara nyingi hutumia mandhari na midundo inayofanana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *