Mke wa Bahati, Diana B, amevunja ukimya wake baada ya kupotea kwenye mitandao ya kijamii kwa takriban mwezi mmoja, akifichua sababu zilizomfanya achukue hatua hiyo ya ghafla.
Kupitia ujumbe wake wa kurejea mtandaoni, Diana amesema aliamua kujiondoa kimya kimya na kufuta machapisho yake yote kwa sababu alihitaji muda wa kujitafakari na kujijenga upya kiakili na kihisia.
Kwa mujibu wake, kelele za mitandaoni, maoni ya watu na presha ya maisha ya umaarufu wakati mwingine humfanya mtu ajisahau, hivyo aliona ni vyema kujiweka mbali na macho ya umma na kuanza upya akiwa na mtazamo tofauti.
Katika hatua nyingine, mama huyo wa watoto watatu amezima tetesi za ujauzito kwa kuchapisha picha na video zikimuonesha akiwa katika umbo lake la kawaida.
Hatua yake ya kufuta kila kitu kwenye akaunti zake na kukaa kimya iliibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki wake, huku baadhi wakihisi huenda alikuwa na ujauzito.