LifeStyle

Emmy Kosgei Azua Gumzo Kuhusu Maisha ya Wachungaji Nairobi

Emmy Kosgei Azua Gumzo Kuhusu Maisha ya Wachungaji Nairobi

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili, Emmy Kosgei, amezua mjadala mzito baada ya kudai kuwa baadhi ya wachungaji jijini Nairobi wanaishi maisha ya anasa yanayokinzana na mafundisho wanayohubiri makanisa siku za Jumapili.

Akizungumza kufuatia mazungumzo aliyoyapata akiwa safarini kwa ndege, Kosgei amesema alipata simulizi kutoka kwa mhudumu wa ndege (air hostess) aliyedai kuwa wachungaji wengi wanapenda kula bata na warembo katika vilabu vya kifahari vilivyopo maeneo ya matajiri jijini Nairobi.

Kwa mujibu wa Kosgei, madai hayo yanapaswa kuwafanya waumini kuwa waangalifu na kuepuka tabia ya kuhukumu wengine kirahisi. Ameonya kuwa endapo Mungu angefunua maisha ya faragha ya watu wengi, basi Wakristo wengi wangeshindwa kusimama imara mbele ya hukumu hiyo.

Mwimbaji huyo ameongeza kuwa mara nyingi watu wanaowakosoa au kuwahukumu wengine huwa na mapungufu yao binafsi, ambayo wakati mwingine ni makubwa zaidi kuliko yale wanayoyalaumu kwa wengine.

Kauli za Emmy Kosgei zimeibua hisia mseto mitandaoni, huku baadhi ya watu wakiona amegusa ukweli mchungu unaopaswa kujadiliwa, na wengine wakihisi madai hayo yanapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari kubwa ili kulinda heshima ya taasisi za kidini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *