Entertainment

KRG The Don Amtupia Maneno Mazito Redsan kwa Kudharau Tuzo yake

KRG The Don Amtupia Maneno Mazito Redsan kwa Kudharau Tuzo yake

Msanii wa dancehall nchini Kenya KRG The Don amejibu mashambulizi ya maneno kutoka kwa mkongwe wa muziki wa reggae na dancehall Redsan baada ya kubezwa mtandaoni kufuatia ushindi wake katika tuzo za Kenya C Awards.

Akijibu kupitia mitandao ya kijamii, KRG hakusita kumshambulia Redsan kwa maneno makali, akisema mara ya mwisho kumuona mkongwe huyo ilikuwa katika ukumbi wa mazoezi (gym) alipokuwa akifanya mazoezi kwa bidii akidaiwa kujiandaa kwa kazi ya ubaunsa.

KRG hakuishia hapo, alienda mbali zaidi kwa kujitolea kumpeleka Redsan vacation ikizingatiwa kuwa kazi aliyokuwa akisaka ya ubaunsa iligonga mwamba.

KRG alitangazwa kama Kenya Dancehall Artist of the Year, ushindi uliibua mjadala mkubwa mitandaoni. Baadhi ya wadau walionekana kutoridhishwa na matokeo hayo, huku Redsan akitoa kauli ya kejeli iliyotafsiriwa na wengi kama dhihaka dhidi ya ushindi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *