Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize, ameibua mjadala mkali mitandaoni baada ya kutoa onyo kali kwa watu wanaoendelea kumhusisha na Diamond Platnumz au kudai kwamba mafanikio yake yanatokana na msaada wa msanii huyo.
Harmonize ameeleza kuwa kitendo cha baadhi ya watu kumweka chini ya Diamond ni kumvunjia heshima, akisisitiza kuwa yeye ni staa mkubwa kuliko Diamond na kwamba safari yake ya muziki imejengwa na juhudi zake mwenyewe.
Amesema kuwa tayari amezungumza na mawakili wake, na mtu yeyote atakayemtaja katika muktadha wa kudai alisaidiwa na Diamond au kumhusisha na msanii huyo kwa namna yoyote, atamchukulia hatua kali za kisheria.
Katika maelezo yake, Harmonize ameongeza kuwa Diamond hastahili heshima anayopewa kuhusu mafanikio yake kwa sababu ndiye aliyempeleka BASATA na kumtaka alipe milioni 600 bila huruma, na jambo hilo alilitekeleza.
Amedai pia kuwa Diamond amekuwa akifurahia changamoto na anguko lake, hali inayomfanya asitake tena jina lake lihusishwe na msanii huyo.