Entertainment

Mdau wa Burudani Awataka Watanzania Kuwasamehe Wasanii Waliojihusisha na Siasa

Mdau wa Burudani Awataka Watanzania Kuwasamehe Wasanii Waliojihusisha na Siasa

Mdau wa burudani nchini Tanzania, Majizzo, ametoa wito kwa wananchi kuwasamehe wasanii waliowahi kujihusisha na siasa, akisema ni muhimu kurejesha mshikamano kati ya mashabiki na tasnia ya sanaa.

Kwa mujibu wa mdau huyo, sekta ya sanaa na burudani imeajiri vijana wengi na imekuwa chanzo kikuu cha kipato kwa familia nyingi. Hivyo, kususia shughuli za burudani kunahatarisha ajira za maelfu ya vijana walioko kwenye tasnia hiyo.

Majizzo, amesisitiza kuwa wasanii ni sehemu ya jamii na mara nyingi hujikuta wakivutwa na mazingira ya kisiasa, lakini mchango wao katika kuendeleza burudani na ajira hauwezi kupuuzwa.

Aidha, mdau huyo ameongeza kuwa endapo hali ya kususia shughuli za sanaa itaendelea, tasnia ya muziki na burudani kwa ujumla inaweza kudorora, jambo litakalowaathiri wasanii, mashabiki na vijana wengi waliopata ajira kupitia sekta hiyo.

Wito huo umetolewa baada ya wananchi wengi kuonekana kususia kabisa shughuli za burudani, wakihisi wasanii wao waliwasaliti kwa kushiriki katika siasa zilizochangia taifa hilo la Afrika Mashariki kutumbukia kwenye machafuko kufuatia uchaguzi wa Oktoba 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *