Gossip

KRG The Don Aahidi Kutoa Msaada kwa Wasanii wa Bongoflev

KRG The Don Aahidi Kutoa Msaada kwa Wasanii wa Bongoflev

Msanii na mfanyabiashara wa Kenya, KRG The Don, ametangaza mpango wa kutoa msaada wa kifedha kwa baadhi ya wasanii wa Bongo wanaodaiwa kukumbwa na changamoto baada ya mashabiki kuwageuka.

Kupitia chapisho lake la Instagram, KRG The Don ameweka video akionekana ndani ya gari akiwa na vibandu vya pesa vinavyokadiriwa kufikia shilingi milioni 10 za Kenya, akisema fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuwasaidia wasanii waliopatwa na ugumu wa kimaisha.

Katika ujumbe wake, KRG amesema anajiandaa kusafiri kuelekea Tanzania kwa lengo la kukutana na wasanii hao na kuwapatia msaada wa kifedha utakaowasaidia kujiendeleza, hasa katika kipindi hiki ambacho baadhi yao wanaripotiwa kukosa maonesho na kupungua kwa sapoti ya muziki wao.

Hatua hiyo inakuja baada ya mashabiki wa Tanzania kususia shows na nyimbo za baadhi ya wasanii, wakidai kutoridhishwa na msimamo wao wa kisiasa, hasa kufuatia uchaguzi wa Oktoba 28 uliogubikwa na mijadala na mvutano wa kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *