Entertainment

Msanii Christina Shusho Amuenzi Raila Kupitia Wimbo Maalum wa Faraja

Msanii Christina Shusho Amuenzi Raila Kupitia Wimbo Maalum wa Faraja

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Christina Shusho, ameachia wimbo maalum wa kumuomboleza kiongozi wa kisiasa hayati Raila Odinga, alioupa jina “Pumzika Baba.”

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shusho ameeleza kuwa Kenya ina nafasi maalum katika huduma yake ya muziki, akisema kuwa taifa hilo limekuwa sehemu muhimu ya mafanikio yake.

Hitmaker huyo wa Shusha Nyavu, ameongeza kuwa ameguswa na msiba huo na alihisi ni wajibu wake kutoa mchango wa faraja kupitia muziki.

Christina Shusho anakuwa msanii wa kwanza kutoka Tanzania kuachia rasmi wimbo wa kumuomboleza Raila, hatua ambayo imepokelewa kwa hisia kali na mashabiki kutoka pande zote mbili za mpaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *