Entertainment

Rapa King Kaka Aachia Wimbo ‘Baba’ Kumuenzi Raila Odinga

Rapa King Kaka Aachia Wimbo ‘Baba’ Kumuenzi Raila Odinga

Rapa wa Kenya King Kaka amejiunga na wasanii wengine katika kumuomboleza na kumuenzi hayati Raila Odinga kwa kuachia wimbo mpya uitwao “Baba.”

Kupitia wimbo huo, King Kaka ameelezea heshima na upendo wake kwa kiongozi huyo mkongwe wa siasa, akisisitiza mchango wake mkubwa katika kupigania haki, demokrasia na umoja wa taifa.

King Kaka anajiunga na wasanii wengine waliotoa kazi za kumkumbuka Raila akiwemo Bahati, Akothee, na Prince Indah, ambao wote wameonyesha kuguswa na kifo cha kiongozi huyo aliyeheshimika kote barani Afrika.

Mashabiki wamempongeza msanii huyo kwa hatua yake ya kutumia muziki kuenzi maisha na urithi wa Raila, wakisema wimbo huo umebeba hisia za taifa zima lililo katika majonzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *