LifeStyle

Nicholas Kioko na Wambo Watumia Helikopta Kwenye Gender Reveal, Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kike

Nicholas Kioko na Wambo Watumia Helikopta Kwenye Gender Reveal, Watangaza Wanatarajia Mtoto wa Kike

Wanandoa maarufu mitandaoni nchini Kenya, Nicholas Kioko na Wambo Ashley, wamevutia hisia za wengi baada ya kuandaa sherehe ya kifahari ya kutangaza jinsia ya mtoto wao, wakitumia helikopta (chopper) katika tukio lililojaa burudani.

Kupitia video na picha walizoshiriki mitandaoni, wanandoa hao walionekana wakiwa katika hafla hiyo ya kipekee ambapo helikopta iliruka juu ya eneo la tukio na kumwaga moshi wa rangi ya pink, ishara iliyothibitisha kuwa wanatarajia mtoto wa kike.

Nicholas Kioko na Wambo Ashley wameelezea furaha yao kubwa kwa baraka hiyo, wakishukuru Mungu na kuwashukuru mashabiki wao kwa upendo na sapoti waliyoendelea kuwaonesha tangu walipotangaza ujauzito huo.

Gender reveal hiyo ya kifahari imezua mjadala mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakiwapongeza kwa ubunifu na uwezo wao wa kuandaa tukio la kiwango cha juu, huku wengine wakijadili mwenendo unaokua wa watu mashuhuri kutumia gharama kubwa katika sherehe za binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *