Entertainment

Pastor T Amkosoa Bahati Baada ya Wimbo Wake “Seti” Kuzua Mjadala Mkali

Pastor T Amkosoa Bahati Baada ya Wimbo Wake “Seti” Kuzua Mjadala Mkali

Mhubiri maarufu Pastor T Mwangi amemtolea uvivu msanii Bahati kufuatia wimbo wake “Seti”, ambao umekosolewa na sehemu kubwa ya Wakenya kwa maudhui yake yanayoonekana kuwa ya utata na ukosefu wa maadili.

Kwenye video inayosambaa mtandaoni, Pastor T amesema kuwa amesikitishwa na mwelekeo wa Bahati na wasanii wengine wanaotumia maudhui tata ili kupata umaarufu wa haraka. Ameeleza kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuona mtu mzima akitengeneza wimbo unaofanana na ponografia, mradi tu watu wazungumzie kazi yake mtandaoni.

Kwa mujibu wa Pastor T, tabia kama hiyo haina tija kwa jamii, na hata kama msanii hatalipa gharama moja kwa moja, ni watoto wake wanaoweza kuathirika baadaye kutokana na matendo hayo.

Mhubiri huyo ambaye miaka ya nyuma alikuwa msanii wa nyimbo za Injili, ameongeza kuwa sanaa inapaswa kutumika kuelimisha na kuinua maadili, siyo kupotosha kizazi cha vijana kwa maudhui yanayokosa heshima.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Bahati kujigamba kuwa amevunja rekodi ya kutazamwa zaidi kwenye YouTube ndani ya saa 48 kupitia wimbo huo “Seti”, licha ya kupingwa vikali na mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *