Entertainment

Rayvanny amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo ya Next Level Music.

Rayvanny amtambulisha msanii mpya ndani ya lebo ya Next Level Music.

Mkurugenzi wa Lebo ya Next Level Music na msanii wa Bongofleva, Rayvanny, amemtambulisha msanii mpya atakayekuwa chini ya usimamizi wa lebo hiyo baada ya kutemana na msanii wake wa kwanza Mac Voice.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Rayvanny ameposti video ikimwonyesha akiwa kwenye maandalizi ya picha (photoshoot) na msanii huyo mpya anayejulikana kwa jina la Kuss Love.

Katika ujumbe wake, Chui amemkaribisha rasmi Kuss Love kwenye familia ya Next Level Music, hatua inayozua matumaini mapya kwa mashabiki wa lebo hiyo.

Kutambulishwa kwa Kuss Love kunakuja wakati ambapo aliyekuwa msanii wa kwanza wa lebo hiyo, Mac Voice, kutemana na Rayvanny kwa madai ya kudhulumiwa kifedha licha ya juhudi zake na mikataba waliyosaini awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *