Entertainment

Watanzania Waanza Ku-unfollow Wasanii Waliomuunga Mkono Rais Samia Suluhu

Watanzania Waanza Ku-unfollow Wasanii Waliomuunga Mkono Rais Samia Suluhu

Baadhi ya Watanzania wameanzisha kampeni kubwa ya mitandaoni ya kuwa-unfollow wasanii maarufu waliomuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika harakati zake za kurejea madarakani.

Miongoni mwa waliokumbwa na wimbi hilo ni staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, ambaye inaripotiwa amepoteza zaidi ya wafuasi 100,000 ndani ya saa 12 pekee. Msanii mwingine anayelengwa ni Harmonize, ambaye naye amekuwa mhanga wa hasira za mashabiki mitandaoni.

Watanzania wengi wanawalaumu wasanii hao kwa kutumia ushawishi wao na majukwaa yao ya kijamii kuiunga mkono serikali wanayoitaja kuwa kandamizi inayoongozwa na Rais Suluhu Hassan.

Hata hivyo, mjadala mkali umeibuka mitandaoni baadhi wakisema wasanii wana haki ya kuwa na misimamo yao ya kisiasa, huku wengine wakisisitiza kwamba mastaa wanapaswa kusimama na wananchi nyakati za migogoro ya kisiasa.

Kampeni hiyo ya kufuta ufuasi au Ku-unfollow imekuja wakati ambapo hali ya kisiasa nchini Tanzania imezidi kuwa tete, kufuatia maandamano na mvutano unaoendelea baada ya matokeo ya uchaguzi yaliyokumbwa na utata mkubwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *