Entertainment

Wema Sepetu Ajaza Fedha Kwenye Kapu la Lady Jaydee Jukwaani

Wema Sepetu Ajaza Fedha Kwenye Kapu la Lady Jaydee Jukwaani

Staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu, amewaacha wengi midomo wazi baada ya kuonyesha upendo wa dhati kwa mwanamuziki mkongwe Lady Jaydee wakati wa tamasha la Valentine lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika usiku huo wa mahaba, uliopambwa na burudani kutoka kwa Lady Jaydee na bendi yake, Wema Sepetu alionekana kuguswa na wimbo uitwao “Siwema ulivyopigwa live jukwani”, kitendo kilichomfanya kunyanyuka alikokuwa amekaa na kuanza kutembea kwa madaha kuelekea jukwaani huku akishangiliwa na mashabiki.

Akiwa mbele ya Lady Jaydee na bendi yake, Wema alianza kutupa noti moja moja ndani ya kapu hadi pomoni, kitendo kilichoashiria kuguswa kwake na wimbo huo pamoja na heshima aliyonayo kwa msanii huyo. Lady Jaydee naye alionekana kufurahia tukio hilo huku akiendelea kuimba bila kukatiza burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *